Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 6 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Oktoba 2026
Jumanne · Juma la 27 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 27 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Bruno, padre · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
13Mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya nyuma katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyokuwa nikilitesa kwa ukali kanisa la Mungu zaidi ya kipimo na kuliteketeza. 14Nilikuwa nimeendelea katika Dini ya Kiyahudi zaidi ya ndugu zangu wengi Wayahudi. Nilikuwa na bidii sana katika tamaduni za baba zangu. 15Lakini Mungu alipendezwa kunichagua mimi kutoka tumboni mwa mama. Aliniita mimi kupitia neema yake 16kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili kwamba nimtangaze yeye miongoni mwa watu wa mataifa. Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu 17na sikupanda kwenda Yerusalem kwa wale waliokuwa mitume kabla yangu. Badala yake nilienda Uarabuni na baadae kurudi Damesiki. 18Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kumtembelea Kefa, nikakaa naye kwa siku kumi na tano. 19Lakini sikuona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndungu yake na Bwana. 20Tazama, mbele za Mungu, sidanganyi kwa kile niandikacho kwenu. 21Kisha nilikwenda mikoa ya Shamu na Kilikia. 22Sikuwa najulikana kwa macho kwa makanisa ya Uyahudi yale yaliyokuwa katika Kristo, 23lakini walikuwa wakisikia tu, “Yeye aliyekuwa akitutesa sasa anatangaza imani aliyokuwa akiiharibu.” 24Walikuwa wakimtukuza Mungu kwa ajili yangu.
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya daudi. Ee Yahwe, wewe umenichunguza, na unanijua. 2Wewe unajua nikaapo na niinukapo; unayajua mawazo yangu tokea mbali sana. 3Unachunguza wenendo wangu na kulala kwangu; unazijua njia zangu zote. 13Wewe uliumba sehemu zangu za ndani; uliniumba tumboni mwa mama yangu. 14Nitakusifu, kwa maana nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu. Nafsi yangu yalijua hili vizuri sana. 15Mifupa yangu haikusitirika kwako nilipoumbwa kwa siri, nilipoumbwa kwa ustadi pande za chini za nchi.
Injili
38Sasa walipokuwa wakisafiri, waliingia katika kijiji fulani, na mwanamke mmoja jina lake Martha alimkaribisha nyumbani kwake. 39Alikuwa na dada aliyeitwa Mariamu, aliekaa miguuni pa Bwana na kusikiliza neno lake. 40Lakini Martha alijipa shughuli nyingi za kuandaa mlo. Alikwenda kwa Yesu, na kusema, “Bwana, haujali kwamba dada yangu ameniacha nihudumu peke yangu? Hivyo basi mwambie anisaidie.” 41Lakini Bwana alimjibu na kumwambia, “Martha, Martha, una sumbuka juu ya mambo mengi, 42lakini ni kitu kimoja tu cha muhimu. Mariamu amechagua kilicho chema, ambacho hakitaondolewa kutoka kwake.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Bruno, padre
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki