Gundua › Kwa mahujaji › Sinai › Oasisi ya Feiran
Sinai · Kituo cha 3 · Siku ya 1
Oasisi ya Feiran
mita 852 juu ya usawa wa bahari
Katika Biblia
Huko Refidimu hapakuwa na maji; watu waligombana na Musa, na kwa neno la Yahweh aliupiga mwamba huko Horebu, na maji yakatoka ndani yake.
Jamii yote ya Israeli ili safiri kutoka nyikani ya Sinu, wakifuata maelekezo ya Yahweh. Walieka kambi Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa. Hivyo watu wakamlaumu Musa kwa hali yao na kusema, “Tupe maji ya kunywa.” Musa akasema, “Kwanini mnagombana na mimi? Kwanini mnajaribu Yahweh?” Watu walikuwa na kiu sana, na waka mlalamikia Musa. Wakasema, “Kwanini umetutoa Misri? Ili utuue sisi na watoto wetu na mifugo yetu kwa kiu?” Kisha Musa akamlilia Yahweh, “Nini ni fanya kwa hawa watu? Wako tayari ata kunipiga mawe.” Yahweh akamwambia Musa, “Nenda mbele yao, na uchukuwe baadhi ya wazee wa Israeli. Chukuwa gongo ulilo piga nalo mto, na uende. Nitasimama mbele yako pale kwenye mwamba wa Horebu, na utaupiga mwamba. Maji yatatoka ya watu kunywa.” Kisha Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli. Aliita ile sehemu Massa na Meriba kwasababu ya malalamishi ya Waisraeli, na kwasababu walimjaribu Bwana kwa kusema, “Je Yahweh yupo miongoni mwetu au hapana?”Mapokeo
Kwa mujibu wa mapokeo moja, oasisi hii ndiyo Refidimu. Hapa palisimama Farani, mji uliokuwa na askofu wake katika enzi za Bizanti, ambako Egeria alipumzika; mapokeo mengine yanaweka Refidimu karibu zaidi na mlima.
Hapa leo
Oasisi ndefu zaidi ya Sinai: mashamba ya mitende, bustani za Wabedui, magofu ya Bizanti na nyumba ndogo ya watawa wa kike wa monasteri ya Sinai.
Kwa macho ya mahujaji wa zamani
Basi, tulipokuwa tumefika Farani, ulio umbali wa maili thelathini na tano kutoka Mlima wa Mungu, ilitubidi tukae pale siku mbili ili kurejesha nguvu zetu.Egeria, takriban 381–384 · tafsiri yetu
Kabla ya kusafiri, angalia ushauri wa usafiri wa nchi yako. Saa za kufungua na kanuni za maeneo hubadilika — tazama kurasa zao rasmi.
Mipaka ya nchi kavu: Natural Earth (mali ya umma).