Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sulemani
Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sulemani
Ujenzi wa hekalu waanza
1 Fal 6:1–3 · 2 Nya 3:1–4
1 Fal 6:1–31Kwa hiyo Sulemani akaanza kulijenga hekalu. Hii ilikuwa mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani huko Israeli, katika mwezi wa Ziv, ambao ndio mwezi wa pili.
2Hekalu ambalo mfalme Sulemani alimjengea BWANA lilikuwa na urefu wa mita 27, na upana wa mita 9, na kimo cha mita 13. 5.
3Na ukumbi uliokuwa mbele ya hekalu ulikuwa na urefu wa mita 9 na upana wa mita 4. 5 sawa na upana wa sehemu kuu ya hekalu.
2 Nya 3:1–41Kisha Selemani akaanza kuijenga nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, ambako Yahwe alimtokea Daudi baba yake. Aliandaa sehemu ambayo Daudi aliikusudia, katika sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi.
2Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili, katika mwaka wa nne wa utawala wake.
3Sasa hivi ndinyo vipimo vya ule msingi ambao Selemani alijenga kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Akitumia mtindo wa vipimo vya zamani, urefu ulikuwa mikono sitini, na upana ulikuwa mikono ishirini.
4Urefu wa ukumbi mbele ya nyumba ulikuwa mikono ishirini, ukilingana na upana wa nyumba, urefu wake kwenda juu pia ulikuwa mikono ishirini, na Selemani akaifunika sehemu ya ndani kwa dhahabu halisi.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY