Gundua › Injili kando kwa kando › Mafundisho
Injili kando kwa kando · Mafundisho
Hazina mbinguni
Mt 6:19–21 · Lk 12:33–34
Mt 6:19–2119Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba.
20Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba.
21Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.
Lk 12:33–3433Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa—hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.
34Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY