Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2026 › 12 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 12 Desemba 2026
Jumamosi · Juma la 2 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 2 la Majilio
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: zambarau
Bikira Maria wa Guadalupe · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki, seti kwenye mtindo wa Shoshannim Eduth. Zaburi ya Asafu. Usikie, Mchungaji wa Israel, wewe uliye muongoza Yusufu kama kundi; wewe uketiye juu ya makerubi, utuangazie! 2Machoni pa Efraimu na Benjamini na Manase, uziinue nguvu zako; njoo na utuokoe. 14Urudi, Ee Mungu wa majeshi; kutoka mbinguni utazame chini na uuangalie na kuujali huu mzabibu. 15Huu ni mzizi ambao mkono wako wa kuume umeupanda, mashina ambayo wewe uliyafanya yakue. 17Mkono wako na uwe juu ya mtu aliye mkono wako wa kuume, kwa mwana wa mtu uliyemfanya imara kwa ajili yako mwenyewe. 18Ndipo hatuta kuacha wewe; utuhuishe, nasi tutaliita jina lako.
Injili
10Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, “ Ni kwanini waandishi wanasema kuwa Eliya atakuja kwanza? 11Yesu akawajibu na kusema, “Eliya atakuja kweli na atarudisha mambo yote. 12Lakini naawaambieni ninyi, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua. Badala yake, walimfanyia mambo watakayo wao. Na hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoteswa katika mikono yao.” 13Ndipo wanafunzi wakatambua kuwa alikuwa akiongea habari za Yohana Mbatizaji.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki