Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 11 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 29 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 11 Novemba 2026
Jumatano · Wiki ya 24 baada ya Pentekoste · Sauti ya 6
Sikukuu na watakatifu
Mtawa Mfiadini Anastasia Mroma (karibu 249-259)
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Hatimaye, ndugu, twawatia moyo na kuwasihi kwa Yesu Kristo. Kama mlivyopokea maelekezo toka kwetu namna iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kwa njia hiyo pia muenende na kutenda zaidi. 2Kwa kuwa mwajua ni maelekezo gani tuliyowapa kupitia Bwana Yesu. 3Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Mungu: utakaso wenu - kwamba muepuke zinaa, 4Kwamba kila mmoja wenu anajua namna ya kumiliki mke wake mwenyewe katika utakatifu na heshima. 5Usiwe na mke kwa ajili ya tamaa za mwili (kama Mataifa wasiomjua Mungu). 6Asiwepo mtu yeyote atakaye vuka mipaka na kumkosea nduguye kwa ajili ya jambo hili. Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye kulipa kisasi kwa mambo yote haya, kama tulivyo tangulia kuwaonya na kushuhudia. 7Kwa kuwa Bwana hakutuita kwa uchafu, bali kwa utakatifu. 8Kwa hiyo anayelikataa hili hawakatai watu, bali anamkataa Mungu, anayewapa Roho Mtakatifu wake. 9Kuhusu upendo wa ndugu, hakuna haja ya mtu yeyote kukuandikia, kwa kuwa mmefundishwa na Mungu kupendana ninyi kwa ninyi. 10Hakika, mlifanya haya yote kwa ndugu walioko Makedonia yote, lakini twawasihi, ndugu, mfanye hata na zaidi. 11Twawasihi mtamani kuishi maisha ya utulivu, kujali shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaamuru. 12Fanya haya ili uweze kuenenda vizuri na kwa heshima kwa hao walio nje ya imani, ili usipungukiwe na hitaji lolote.
Injili
9Nami pia nawaambieni, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa. 10Kwa kuwa kila mtu aombaye atapokea, na kila mtu atafutaye atapata, na kila mtu apigaye hodi, mlango utafunguliwa kwake. 11Ni baba yupi miongoni mwenu, mwanaye akimuomba samaki atampa nyoka badala yake.? 12Au akimuomba yai atampa nge badala yake?. 13Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajuwa kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni kwamba atawapa Roho Mtakatifu hao wamuombao?”
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Ibrahimu, mtawa wa faragha, na Mbarikiwa Maria, mpwa wake (karibu 360)
- Mtakatifu Mtawa Ibrahimu, arkimandriti wa Rostov (1073-1077)
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri, na pamoja naye Wafiadini Kosma, Vikta, Naumu, Filipo, Yohana, Paulo, Andrea, Paulo, Basili, Aleksi, Yohana na Mfiadini Agathia (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Yohana, padri (1930)
- Mfiadini wa Kikasisi Eugenio, padri (1937)
- Mfiadini Anastasia (baada ya 1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Leonida, padri (1941)
- Wafiadini Klaudio, Asterio, Neoni na Theonila (285)
- Mtakatifu Mtawa Ana (Eufemiano) (826)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 29 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 11 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki